Mabingwa wa soka nchini Ufaransa, PSG wanajipanga kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Man Utd Anthony Martial.

PSG, wameanza mikakati kwa kufanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji huyo kwa kuamini kutakuwa na uwezekano kwa Martial kurejea nyumbani, baada ya kuondoka mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea AS Monaco.

Gazeti la michezo la nchini Ufaransa (L’Equipe), limeripoti kwamba PSG wametenga kiasi cha Euro milioni 75, kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo ambaye ameonekana kutakata akiwa na Man Utd kwa msimu wa 2015-16.

Hata hivyo imeelezwa kwamba kuna changamoto kubwa kwa PSG juu ya kufanikisha mpango wa kumnasa Martial, kutokana na mshambuliaji huyo kukiri kupendezwa na mazingira ya nchini England.

PSG, wameanza mikakati ya kumsaka mchezaji anayecheza nafasi ya ushambuliaji, kufutia Zlatan Ibrahimovic kumaliza mkataba na klabu hiyo na ameshaweka msimamo wa kusaka mahala pengine pa kucheza soka lake kwa msimu wa 2016-17.

Kikosi Cha Serengeti Boys Chatakata Mbele Ya Wenyeji
Callum Wilson, Matt Ritchie Wawanyima Usingizi West Ham Utd

Comments

comments