Nyota wa Brazil Neymar da Silva Santos Júnior, ameripotiwa kukubali kijiunga na matajiri wa jijini Paris nchini Ufaransa Paris Saint-Germain, ambao wameonyesha nia ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki cha majira kiangazi.

Esporte Interativo wameripoti taarifa za mshambuliaji huyo wa FC Barcelona kukubali maslahi binafsi na klabu ya PSG, huku ada yake ya uhamisho ikitajwa kufikia Euro milioni 222.

Uongozi wa FC Barcelona nao unatajwa kuwa tayari kufanya biashara ya kumuuza Neymar, kutokana na uwepo wa taarifa za kuikubali ofa iliyotumwa na PSG, ambao kwa misimu miwili wamekua wakimunda mshambuliaji huyo.

Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Esporte Interativo Marcelo Bechler,‏ amesema tayari pande hizo mbili zimeshakutana na kufanya makubaliano ya awali, na wakati wowote ndani ya juma moja ama majuma mawili dili la usajili wa Neymar litakamilishwa na kutangazwa hadharani.

Maamuzi ya usajili wa Neymar yanafanywa na viongozi wa PSG, huku ikiwa tayari wameshakamilisha dili la kumsajili beki wa kulia kutoka nchini Brazil Dani Alves, aliyeachana na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC.

Neymar, mwenye umri wa miaka 25, alihamia FC Barcelona mwaka 2013 akitokea Santos Futebol Clube ya nchini kwao Brazil, na mpaka sasa amesaidia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa La Liga mara mbili, kombe la Mfalme (Copa del Rey) mara tatu na ligi ya mabingwa barani Ulaya mara moja.

Lucas Leiva Atambulisha SS Lazio
Video: mimi nilishakuwa maarufu kabla ya Yanga-Jerry