Wakati mashabiki wa masumbwi duniani wakihesabu saa kadhaa kushuhudia pambano la uzito wa juu la ubingwa wa dunia kati ya mabingwa ambao hawajawahi kupigwa, Anthony Joshua na Joseph Parker, wawili hao wamechochea kuni kwenye moto wa pambano lao.

Parker aliyetua Uingereza juzi akitokea nchini kwao New Zealand amesema kuwa wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari, alimuona Joshua akiwa mwenye hasira dhidi yake.

“Nilichokiona usoni kwake ni hasira, ana hasira na niliweza hata kuihisi kwa kuangalia lugha ya mwili na hata alikuwa mzito kunipa mkono,” alisema Parker.

Bondia huyo alidai kuwa atafanya kile anachokiweza kwa mtindo tofauti kuhakikisha anarudi na mikanda yote nchini kwao.

Naye Joshua ambaye anapewa nafasi kubwa ya ushindi katika pambano hilo litakaloshuhudiwa na zaidi ya watu 80,000 ndani ya uwanja wa mpira huko Cardiff, alisema kuwa ana uhakika atampiga mpinzani wake kati ya raundi ya 8-10, ingawa amejiandaa kwa raundi zote 12.

Pambano hilo litafanyika leo usiku na kuoneshwa na kituo cha runinga cha Sky Sports.

Askofu awashauri wakristo wanayepaswa kumchagua uchaguzi ujao
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 31, 2018