Wafanyabiashara katika soko la Mwananyamala Mapinduzi wamesemabkuwa hali ya biashara kwa msimu huu wa sikukuu ya Pasaka 2021 imekuwa chini sana na kupelekea hali ya biashara kuwa ngumu.

Wakizungumza na Dar24 baadhi ya wafanyabiashara wemetaja maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli kuwa miongoni mwa sababu ambazo zimechangia ugumu wa biashara kwa msimu huu.

Mbali na kuwa katika kipindi cha maombolezo, wafanyabiashara hao wameleza kuwa biasharahuwa jambo la msimu na wakati mwingine hupanda na kushuka, huku wakibainisha kuwa sikukuu ya mwaka huu imekuwa tofauti na miaka iliyopita ingawa bado wanapata faida.

Aidha wafanyabiashara hao wamesema kuwa kinachotakiwa kufanyika ni kupambana na kuendelea na biashara ili kuweza kukabiliana na hali hiyo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 4, 2021
Ajali ya treni yaua zaidi ya 50, Taiwan yaomboleza