Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa pato la taifa limeongezeka kwa shilingi trilioni 47.1 mwaka 2016 mpaka Shilingi trilioni 50.5 kwa mwaka 2017.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akieleza mwenendo wa uchumi kwa mwaka 2017 huku akibainisha kuwa pato la kila mwananchi limeongezeka.

“Kutokana na kuimarika kwa pato la taifa, hata pato la mtu mmoja mmoja nalo limeimarika na pato la kila mwananchi limeongezeka kutoka Shilingi milioni 2.1 mwaka 2016 mpaka Shilingi milioni 2.3 kwa mwaka,”amesema Dkt. Mpango.

Hata hivyo, Dkt. Mpango amesema kuwa sekta zilizochangia kuimarika kwa pato hilo ni uchimbaji madini na mawe iliyokua kwa asilimia 17.5, uchukuzi na usafirishaji mizigo asilimia 16.6 na habari na mawasiliano asilimia 14.7

Viongozi wa dini watakiwa kufundisha madili mema
Video: Jeshi la polisi lathibitisha usalama na ulinzi sikukuu ya Eid El-Fitri