Mshambuliaji wa klabu ya Sao Paulo, Alexandre Pato amepasua ukweli wa mambo yaliyokua yamejificha wakati wa dirisha la usajili lilifungwa mwishoni mwanzoni mwa mwezi huu huko nchini England.

Mshambuliaji huyo ambaye alipatra nafasi ya kuitumikia klabu ya AC Milan kati ya 2007–2012, amesema huenda angerejea barani Ulaya akitokea nchini kwao Brazil, baada ya wawakilishi wa klabu ya Man Utd kumfuatilia daikika za mwisho kabl ya dirisha la usajili halijafungwa, lakini aliweka msimamo wa kutotaka mazingira ya soka lake kwa sasa kuwa nje ya nyumbani kwao.

Amesema saa mbili kabla ya dirisha halijafungwa, wawakilishi wa Man Utd walikuwa na mazungumzo na wakala wake na walihimiza kukamilishwa kwa dili ya kusajili kwenye klabu hiyo, lakini msimamo alishikilia msimamo wake wa kutotaka kurejea barani Ulaya.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kwa sasa yupo kwenye klabu ya Sao Paulo kwa mkopo na mwishoni mwaka huu anatarajiwa kurejea kwenye klabu yake ya Corinthians ambayo imeonyesha nia ya kuwa tayari kumuuza.

Man Utd walionyesha dhahir kuhitaji mshambuliaji baada ya kukubali kuwaachia Robin van Persie, Javier Hernandez pamoja na Radamel Falcao aliyekua kwa mkopo huko Old Trafford.

Hata hivyo Man Utd walifanikisha zoezi la kuziba nafasi ya ushambuliaji klabuni hapo, baada ya kumsajili Anthony Martial aliyetokea AS Monaco kwa ada ya paund million 36 ambazo ni sawa na Euro milion 58.

Zico Alia Na Kanuni Za Uchaguzi FIFA
Roberto Firmino Aondolewa Kikosini