Mabingwa wa soka Tanzania Bara Wekundu Wa Msimbazi Simba leo wamemtambulisha Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ambaye anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Mfaransa Pierre Lechantre, aliyeondoka nchini mwezi uliopita.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mabosi wa Simba kugoma kumuongezea mkataba Lechantre ambaye alipewa timu kwa muda wa miezi sita pekee na baada ya kumalizika wakaacha naye.

Kocha Aussems aliyewahi kuzinoa timu kadhaa zikiwamo za Ligi Kuu ya Ufaransa, ES Toyes AC na Stade de Reims pamoja na mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2012, AC Leopards ya Congo, ametambulishwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika heteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Kabla ya kutambulishwa rasmi, kocha huyo mwenye umri miaka 53 na aliyecheza kama beki enzi zake za uchezaji akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 3, alisaini mkataba wa mwaka mmoja na uongozi wa klabu ya SImba ambao umewakilishwa na kaimu rais Salim Abdallah (tray Again).

Simba wamefikia hatua ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuridhishwa na CV zake hivyo kuona anastahili kukinoa kikosi hicho ambacho kimeshiriki michuano ya SportPesa Super CUP na KAGAME bila ya Kocha Mkuu.

Wakati Aussems akimwaga wino, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuweka kambi nchini Uturuki kwa majuma mawili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi utaoanza Agosti 22.

Video: Steve Nyerere amjibu Muna Love
Steve Nyerere ajibu shambulio la Muna 'nimesamehe'