Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kumalizika kwa mashindano ya Olimpiki 2016 inayofanyika Rio, Polisi nchini Brazil wamemkamata Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Ulaya, Patrick Hickey kwa kosa la kuuza tiketi kinyume na makubaliano.

Inaripotiwa kuwa Hickey alikamatwa na Polisi baada ya kugundulika kuwa alikuwa akiuza tiketi za Olimpiki kwa gharama kubwa tofauti na bei inayotakiwa.

Katika taarifa ambayo imetolewa na Polisi wa nchi hiyo inaeleza kuwa wakati wakitaka kumkamata mtu Hickey alijaribu kuwatoroka lakini walifanikiwa kumkamata wakati alipotaka kuwakimbia kutoka katika chumba chake na kuhamia chumba kingine cha hoteli.

Hata hivyo vyombo vya habari vya Brazil vinaamini kuwa sababu ya kukamatwa Hickey ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Olimpiki la Irenland (OCI) inahusiana na MuIreland mwenzake, Kebin James Mallon ambaye alitiwa mbaroni na Polisi siku ya ufunguzi wa michezo hiyo.

Paul Pogba: Nipo Tayari Kuwakabili Southampton
Kingsley Coman Kukaa Nje Majuma Manne Hadi Manane