Kocha mkuu wa kikosi cha New York City FC Patrick Vieira, kwa mara ya kwanza amezungumzia safari yake ya kutimiza ndoto za za kuwa mkuu wa benchi la ufundi akimuhusha aliyekua bosi wake wakati akicheza soka Arsene Wenger.

Vieira, ambaye ni mmoja wa wachezaji waliopata mafanikio makubwa wakiwa na kikosi cha Arsenal, hususan kutwaa ubingwa wa ligi ya England bila kufungwa wakati wa msimu wa 2003/04, alianza kufuata ndoto za kutaka kuwa mkuu wa benchi la ufundi akiwa na kikosi cha Man City na hatimae kukabidhiwa kikosi cha klabu ya New York City FC ambayo inamilikiwa na Taykun Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan.

“Sikuwahi kusema Arsene hakunipa mipango ya kuwa kocha wa soka. Aliwahi kufanya hivyo lakini bila kutilia mkazo wa mara kwa mara, na kwa upande wangu sikutilia maanani kwa kipindi hicho,” Vieira Aliliambia jarida la France Football.

“Labda Arsene alitaka wachezaji wake wote wawe katika mlolongo wa kuongoza soka katika maisha yao kwa malahi fulani.”

Aliongeza kuwa: “Inasikitisha kuona baadhi ya wachezaji wa zamani wa Arsenal ni sehemu ya wafanyakazi katika benchi la ufundi la klabu hiyo, lakini kwangu imeshindikana kuwa hata msaidizi wa kikosi cha kwanza.”

Kabla ya kuwa kocha wa New York City FC inayoshiriki ligi ya nchini Marekani (MLS), Vieira alikua kocha wa kikosi cha vijana cha Man City baadae alipandishwa chezo na kukiongoza kikosi cha wachezaji wa akiba.

Video:Machinga ilala kuhamishiwa masoko mapya
Mwamuzi Wa Kike Tanzania Kuchezesha Afcon Ya Kinamama