Aliyekua nahodha na kiungo wa kutumainiwa wa klabu ya Arsenal, Patrick Vieira ameteuliwa kuwa meneja wa kikosi cha klabu ya New York City inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani MLS.

Vieira mwenye umri wa miaka 39, amesaini mkataba wa miaka mitatu kukinoa kikosi cha klabu hiyo, ambayo ina uhusiano na mmiliki wa klabu ya Man City ya nchini England.

Kabla ya kufikia hatua ya kuajiriwa na klabu ya New York City, Vieira alikua anakifundisha kikosi cha vijana chini ya umri wa 21 cha Manchester City.

Viera pia anaendelea kukumbukwa katika soka la dunia, kufuatia kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambacho kilitwaa ubingwa wa kombe la dunia 1998, kwa kuifunga timu ya taifa ya Brazil mabao matatu kwa sifuri.

Vieira ataanza kuwajibika huko nchini Marekani tarehe mosi mwezi januari mwaka 2016, huku jukumu kubwa atakalokua nalo ni kuhakikisha klabu ya New York City inafikia malengo ya kushindana na klabu nyingine na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa MLS.

Dk. Shein Maalim Seif Wakutana Kumaliza Mambo
Soka La Ujerumani Laingia Majaribuni