Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amevunja ukimya na kutolea ufafanuzi juu ya kauli aliyoitoa hivi karibuni ya kuwatambua wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambalo limetafsiriwa tofauti kupitia mitandao ya kijamii.

Makonda amesema hakutoa agizo la kuwakamata watu wasio na kazi maalumu bali aliagiza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kwenda nyumba hadi nyumba ili kuwatambua na kufahamu shughuli zinazofanywa na wakazi wa maeneo husika.

“Watu wamefanya upotoshaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, mimi sikusema watu wasio na kazi maalumu wakamatwe, na wala sikutoa tamko kimsingi nilitoa maelekezo kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wapite nyumba hadi nyumba ili waweze kuwatambua wakazi kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kufanikisha mipango ya maendeleo.” alisema Makonda.

Kuhusu kauli aliyoitoa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita kwa kudai agizo hilo ni batili na haliwezi kutekelezeka kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi Makonda amesema jukumu la ulinzi na usalama kwa Mkoa wa Dar es Salaam lipo chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na siyo Meya wala mtu mwingine.

Aidha Makonda amesema operesheni ya kuwaondoa ombaomba wa Jiji la Dar es Salaam bado inaendelea na kusisitiza baada ya miezi mitatu ombaomba wa jiji hili watakwisha kwani yeye ndiye ‘mbabe wa vita’.

 

Tatu Zathibitisha Ushiriki Wa Klabu Bingwa Duniani
Video: Demba Ba Avunjika Mguu Akiwa Vitani