Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda atakua mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Young Africans Jumapili,  Uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.

Tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko(Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.

Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

Habari Picha: Jaji Mkuu aongoza zoezi la upandaji miti jijini Dodoma
Mashabiki, Wanachama wa Simba waombwa kufika Taifa