Kiungo wa Man Utd ambaye pia ndio mchezaji ghali zaidi kwa sasa duniani, Paul Pogba amezungumza kuhusu uwezo wa soka ambao amekuwa akionyesha uwanjani kutokana na kuwa akitupiwa lawama kuwa kiwango chake kimeshuka.

Pogba alisema kumekuwa na watu wakosoaji ambao wamekuwa wakimzungumzia uwezo wake lakini yeye hajali na anadhani anahitaji muda ili kuzoea timu anayoitumikia ya Man Utd.

“Nahitaji muda kidogo kuizoea Manchester, muda ambao mashine itaanza kufanya kazi nitakuwa nimezoea,” alisema Pogba wakati akizungumza na French TV na kuongeza.

“Watu wanapenda kuzungumza kuhusu Pogba, ni wakosoaji kila siku, ila mimi sijali, naweka muziki na kucheza”

Mungai ajivua lawama, Adai elimu ilianza kuporomoka enzi za Kikwete
Zeben: Tulikuwa Na Mchezo Mzuri, Tuliwazidi Kila Kitu Yanga