Wakati huu nyaraka za usajili wake wa Paundi milioni 100 zikithibitishwa kuwasili nchini England, kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Juventus, Paul Pogba ameendelea kujiweka fiti huko Marekani kuelekea msimu mpya wa 2016/2017.

Dili la Pogba kujiunga na Man Utd  linatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia juma hili, lakini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 anaendelea na likizo yake ya majira ya kiangazi mjini New York ambapo jana alionekana akifanya mazoezi ya kupigana ngumi  ‘kickboxing’ .

Pogba ame-post video kwenye akaunti yake ya Twitter ikionesha akipangua ngumi na kumpiga mateke mpinzani wake, huku akiwa amevaliwa vest ya nyota wa Golden State Warriors, Stephen Curry.

Pogba, anatarajiwa kurejea Man Utd kwa dau ambalo litavunja rekodi ya dunia, ingawa bado kuna mjadala mzito kama kiungo huyo ana thamani hiyo ya paundi milioni 100.

Hull City Washindwa Kumpata Chris Coleman
Chelsea Wabuni Mbinu Mpya Ya Kumrejesha Lukaku