Ndoto za usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa, Paul Pogba bado zinaendelea kuwatesa mashabiki wa Man Utd, ambao wana hamu ya kuona zinatimia kwa meneja wao Jose Mourinho kumuhamishia Old Trafford katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Kiungo huyo amekua gumzo kwa miezi miwili sasa, kuhusu safari yake ya kusajiliwa na mashetani wekundu (Man Utd), akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC, lakini kila kukicha pamekua na taarifa tofauti.

Man Utd wameshafikia makubaliano ya awali ya kumsajili kiungo huyo wa Juventus kwa ada ya itakayovunja rekodi ya euro mil 110.

Juventus wamekuwa wakikanusha uvumi wa nyota huyo kuondoka msimu huu, huku pia wakala wake Mino Raiola akikaa kuthibitisha kama uhamisho umekamilika ama la.

Na sasa Pogba, ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni baada ya Michuano ya Euro kumalizika ameposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram yenye maelezo: “we say it all by saying nothing at all #holidays.”

En disant rien on a tout dis ?? we say it all by saying nothing at all #holidays

A photo posted by Paul Labile Pogba (@paulpogba) on

Avamia kituo cha wenye ulemavu na kuua 19 kwa kisu
Mzee wa Upako: Lowassa ni tishio CCM