Mlinda mlango wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Paul Robinson ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 27.

Robinson alianza kucheza mpira katika klabu ya Leeds United mwaka 1998 ametangaza kustaafu baada ya kusumbuliwa na maumivu ya mgongo wakati akiitumikia klabu ya Burnley.

Mbali na kuitumikia klabu ya Leeds na timu ya taifa mlinda mlango huyo pia alizitumikia klabu zaTottenham Hotspur,  Blackburn pamoja na Burnley.

Mchezaji huyo alijiunga na Burnley mwaka 2016 na amekuwa akicheza kama goli kipa msaidizi wa kipa namba moja wa timu hiyo Tom Heaton.

”Nimekuwa na bahati kucheza mchezo ninaoupenda sana kwa muda mrefu,naishukuru familia yangu na marafiki wote waliokuwa na mimi katika kipindi chote” alisema Robinson.

Video: Maimamu watoa neno kwa JPM kuhusu Masheikh wa Uamsho
Associazione Calcio Milan Yakamilisha Kwa Lucas Biglia

Comments

comments