Mshambulaiji wa klabu bingwa nchini Italia Juventus Paulo Dybala ameamsha upya hisia za kutaka kucheza na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Man Utd ya England Paul Pogba.

Dybala ameamsha hisia za kuhitaji kucheza na kiungo huyo, huku taarifa zikieleza kuwa, huenda uongozi wa Juventus ukaomba kikao na Man Utd kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kumrejesha Pogba angalau kwa mkopo itakapofika mwezi Januari mwaka 2019, wakati wa dirisha dogo la usajili.

Dybala amesema ni dhahir amekua akivutiwa na uchezaji wa kiungo huyo na anaamini kama atafanikiwa kurejea mjini Turin, atawezesha mafanikio ya upatikanaji mkubwa mabao.

“Nina shauku kubwa ya kutaka kucheza na Pogba, ni mchezaji wa aina tofauti ambaye amewahi kupita hapa na kupata mafanikio, ana uwezo wa kipekee hasa anapopewa nafasi ya kucheza kwa kujiachia uwanjani.”

“Itakua furaha yangu kubwa kumuona Pogba akirejea hapa na kucheza tena, naamini hata yeye anahitaji iwe hivyo, kwa sababu anafahamu uzuri na ushirikiano uliopo kwenye kikosi cha Juventus,” amesema Dybala.

Kati kati ya juma lililopita Pogba alirejea kwa maraya kwanza Allianz Stadium tangu alipoondoka klabuni hapo mwaka 2016 na kujiungana Man Utd.

Pogba alirejea mjini Turun akiwa na kikosi cha Man utd kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa tano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi, na alifanikiwa kucheza katika mpambano huo uliomalizika kwa Mashetani wekundu kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

 

Suala la Gesi na Mafuta lamuibua Maalim Seif
Kalemani avunja Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA)

Comments

comments