Kiungo mshambuliaji kutoka Hispania na klabu ya Chelsea ya England Pedro Rodriguez, amefanyiwa upasuaji wa bega huku akihusishwa na mipango ya kusajiliwa na klabu ya AS Roma ya Italia.

Kiungo huyo wa zamani wa FC Barcelona alipatwa na majereha ya bega mwishoni mwa juma lililopita, akiwa kwenye mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Arsenal, ambao waliibuka mabingwa kwa kuichabanga Chelsea mabao mawili kwa moja.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Pedro amebainisha kufanikiwa kwa hatua ya upasuaji wa bega lake. “Upasuaji umeenda vizuri, nitarejea hivi karibuni. Ilikuwa vibaya sana kutokushinda Kombe la FA. Nashukuru nyote kwa sapoti yenu.” -Pedro alichapisha kwenye ukurasa wake.

Pedro akitolewa uwanjani baada ya kuumia wakati wa mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Arsenal.

Wakati mkataba wake na Chelsea ukiwa unaelekea ukingoni, Padro anatajwa kuwa yupo tayari kujiunga na AS Roma ya Italia kwa mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zingine zinasema kuwa mchezo wa fainali ya FA dhidi ya Arsenal ambao walipoteza kwa kichapo cha bao mawili kwa moja ulikuwa wa mwisho kwa kiungo huyo ndani ya Chelsea.

Wakati kikosi cha Chelsea kikiwa katika maandalizi ya mpambano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Bayern Munich ya Ujerumani, meneja wa The Blues Lampard awakosa baadhi ya wachezjai wake akiwepo Padro, Pulisic na Cesar Azpilicueta ambao ni majeruhi.

Man Utd wana mlima wa kupanda UEFA Europa League
Jaji Mutungi awaasa CHADEMA kutii sheria za nchi