Bao la ushindi lililofungwa na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Kevin De Bruyne katika dakika za lala salama, wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Man City dhidi ya Sevilla, limepa jeuri, meneja Manuel Pellegrini.

Pellgrini alionekana kuzungumza kwa ujasiri mara baada ya mchezo huo uliounguruma kwenye uwanja wa Etihad mjini Manchester, kwa kusisitiza kikosi chake kimeonyesha uwezo wa kupambana hadi dakika za mwisho.

Meneja huyo kutoka nchini Chile alisema haikuwa imetosha kwa wachezaji wake, pale walipoona mambo yanazidi kuwa magumu kwao huku ubao wa magoli ukisomeka moja kwa moja, lakini ujasiri na uwajibikaji wa kila mmoja ulizaa mafanikio kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 kufunga bao la ushindi.

Pellegrini, ameusifia  ushindi huo kwa kuuita ni wa kishujaa, ambao unawaweka katika mazingira ya kujiamini, kabla ya mchezo wao wa wishoni mwa juma hili ambapo watakuwa wageni wa Man utd kwenye uwanja wa Old Trafford.

Bao la kwanza la Man city katika mchezo huo, lilipachikwa kimiani na beki kutoka nchini Ufaransa Adil Rami, aliyejifunga mwenyewe, huku bao la kujipoza la Sevilla likifungwa na kiungo kutoka nchini Ukraine Yevhen Konoplyanka.

Ushindi huo umeiwezesha Man City kufikisha point 6, kwenye msimamo wa kundi la nne, katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, wakitanguliwa na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus huku nafasi ya tatu ikishikwa na Sevilla wenye point tatu na Borussia Moenchengladbach wanaburuza mkia kwa kumiliki point moja.

 

Idadi Ya Wanaohama Mtwara Kuhofia Vurugu Baada ya Uchaguzi Yaongezeka
FIFA Yamuingiza Kikaangoni Franz Beckenbauer