Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Upendo Peneza kutoka Mkoa wa Geita, leo bungeni amewasilisha hoja binafsi na kusema kuwa elimu bure iende sambamba na utoaji bure wa Pedi kwa wasichana waliopo shule za msingi na sekondari katika shule za umma.

Ambapo ametoa sababu za kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi.

Ametaja sababu hizo ni kwamba wanafunzi hupata hedhi mara moja kwa mwenzi hivyo ni rahisi Serikali kumudu ugawaji wa pedi kila mwezi, kwa kila mwanafunzi.

Pia ametaja kukosa pedi kwa wanafunzi wa kike huchochea  utoro kwa wanafunzi kwa zaidi ya siku 5, kila mwezi, hivyo kwa mwaka mwanafunzi hukosa shule kwa siku 50 ambapo ni sawa na kukosa vipindi 400 kwa mwaka.

Aidha kupitia ukurasa wake wa Twitter, Upendo amemshukuru Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kumuunga mkono na kuona umuhimu wa serikali kutoa pedi bure kwa watoto wakike mashuleni.

Nnape Nnauye katika ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi

@UpendoPeneza

#ElimuBureHaiwezekaniBilaPedi

#FreeEducationFreePads.

 

Dkt. Ndugulile: Hakuna mwanafunzi wa kike aliyezuiwa kusoma
Masauni ajibu tuhuma kamatakamata ya watu kuwekwa ndani zaidi ya masaa 24