Mlimbwende Wema Sepetu amerudi kwenye headlines kwa mara nyingine kufuatia uvumi kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati yake na mwanamuziki maarufu wa Bongo fleva Bob Junior ambaye katika mahojiano yake na mtangazaji Soud Brown amekiri kuwa wawili hao ni wapenzi.

Muda mfupi baada ya mahojiano hayo ya redio kuruka, taarifa hizo zimeenea zikiambatana na kipande kifupi cha video kinachowaonyesha wawili hao wakiwa pamoja katika pozi tofauti tofauti, kiasi cha kuibua gumzo kubwa kote mitandaoni juu ya suala hilo ambalo halikutegemewa na kundi kubwa la mashabiki pamoja na wadau wa wasanii hao.

Hatimaye kuenea kwa kasi kwa video na sehemu ya mahojiano hayo kwenye mtandao wa Instagram huku akisikika Bob Juniour akikiri wazi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo huyo mshindi wa taji la Miss Tanzania mwaka 2006, kumemuibua Wema Sepetu mwenyewe ambaye amejitokeza kupinga vikali kauli za Bob junior na kukanusha taarifa hizo kwa kuweka bayana kile anachodai kuwa ndio ukweli wa dhati kuhusu yeye na mwanamuziki Bob Junior,

Kupitia kwenye ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram, Wema ameandika ujumbe mrefu akifafanua kwa undani kuhusu yeye na Bob Junior na uhalisia wa chanzo cha kurekodiwa kwa video ya pamoja iliyoibua gumzo kote mitandaoni huku akidhihirisha wazi kuchukizwa na kilichotokea.

“Niko disappointed na Bob Junior saaaaanaaa cause maisha yangu always nimekuwa nikimchukulia as a Friend na nimekuwa nikimkubali kama mwana….Sijamuona almost miaka 6 or 7 or even more….Nimekuja kuonana nae juzi & kama kawaida nikawa Excited saaaaaaaanaaaa and nikamchangamkia mno….Na hivyo ndo nilivyo mimi kwa watu woooooote wanaonizunguka na SIWEZI BADILIKA.

Sasa sielewi ndugu yangu ukala nini au umeona ni Sawa kwenda kuongea kuwa mimi ni mwanamke wako. Lini…??? Au ndo Kutafuta kuongelewa yaani ungejua nisivyopenda kuwa kwenye midomo ya watu aisee….Daaaah nimekuwa sad saaaaanaaa maana hata sielewi namwambiaje Mwanaume wangu akanielewa.

Kiukweli umenikosea sana…. Basi kama ni Kick ulikuwa unataka, Si ungenihusisha from the beginning… Tukashauriana…. Haiya Posa hio ya wapi….. Au ulikuwa umelewa. Yaani kuna vitu vinakera sana kwa kweli” ameandika Wema.

Licha ya kuweka wazi kuchukizwa na kilichotokea hasa akimshutumu mwanamuziki Bob Junior kwa kitendo cha kuzungumza maneno anayodai kuwa ni ya uongo, Sepetu amemtumia ujumbe mtangazaji aliyefanya mahojiano na kusambaza sehemu hiyo ndogo anayosikika Bob Junior akizungumza maneno hayo.

“Back to you Soudy, Umeyataka baada ya ku make a Big deal after ile post…Ndugu, mimi kuwa msweet kwa watu vile sio mara ya kwanza. Hata wewe nikikuona nikiwa nakukubali from the heart lazima nikukumbatie na kukukiss, Sio kitu cha ajabu, Ndo nilivyo, Sasa mpaka kufikia kufanyiana Interview wenyewe mjipe Hype na Kick ndo sijaelewa.

Najaribu kuwawazia siwapatii jibu… Posa ipi kwanza, au wewe ndio mshenga…Kutaka kuharibiana tu mahusiano yetu tulionayo…. Sijawapenda hata kidogo…!!! Mna mambo ya Ajabu sana”. ameongeza.

Ukiachilia mbali sakata la Wema na uvumi wa Bob junior ambaye hajasikika akijibu chochote mpaka muda huu, Takribani wiki moja iliyopita mwigizaji Wema Sepetu alishika vichwa mbali mbali vya habari baada kumwaga machozi katikati ya mahojiano na kituo cha televisheni, akirejea kubainisha kufikia hatua ya kupoteza matumaini ya kupata mtoto kutokana na kuhangaika kwa muda mrefu bila mfanikio suala lililogusa hisia za wengi kote mitandao.

Breaking:Mishahara mbioni kupanda, Majaliwa apokea pendekezo
CRB kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi Dodoma