Penzi la Nicki Minaj limetajwa mahakamani kuwa sehemu ya vyanzo vilivyopelekea Rapa Meek Mill kudata na kuvunja masharti ya mahakama na kujiKuta akishushiwa mvua ya hukumu.

Rapa huyo amehumiwa kifungo cha nyumbani cha siku 90 (under house arrest) kilichoambatana na kufungiwa kifaa maalum mguuni (ankle monitor) kitakachokuwa kinaonesha namna anavyopiga hatua zake.

Katika hukumu hiyo, rapa huyo hataruhusiwa kusafiri, kufanya kazi za muziki ikiwa ni pamoja na kutoachia wimbo wowote katika kipindi hicho.

Muendesha mashtaka alilmueleza Jaji Genece Brinkley kuwa Meek Mill alivunja masharti ya kutosafiri aliyopewa baada ya kuachiwa huri. Pia rapa huyo alishindwa katika vipimo vya haja ndogo.

Alisema kuwa Meek Mill alivunja masharti kwa kusafiri kumfuata mpenzi wake Nicki Minaj alipokuwa akifanya matamasha kwenye majiji mbalimbali.

Baadaye, Jaji atafanya tathmini ya siku hizo 90 alizopewa rapa huyo.

 

Wamiliki wa Twitter wapambana na Akaunti za Magaidi wa IS
Baba yake Rihanna ampigia Chapuo Chris Brown kwa mwanae