Mkongwe wa filamu kutoka nchini Marekani, Sylivester Sallon maarufu kwa jina la ‘Rambo’ ameingia kwenye mgogoro na mkewe Flavin, uliopelekea kutengana baada ya takribani miaka 25 ya ndoa yao iliyofungwa mwaka 1997.

“Ninaipenda familia yangu, tunashughulikia masuala haya ya kibinafsi kwa amani na faragha,” Stallone aliiambia CNN.

Inaelezwa kuwa, Flavin aliwasilisha ombi lake la kusitishwa kwa ndoa yao katika Kaunti ya Palm Beach huko Florida nchini Marekani siku ya Ijumaa Agosti 26, 2022, akiomba kuvunjwa kwa ndoa na misaada mingine.

Sylvester Stallone ‘Rambo’ (katikati), akiwa na mkewe Flavin (kulia kwa Rambo), pamoja na watoto wao watatu. Picha na Instagram.

“Ingawa hatutaoana tena, nitathamini uhusiano wa zaidi ya miaka 30 ambao tulishiriki, na najua sote tumejitolea kwa binti zetu warembo, naomba faragha kwa familia yetu tunaposonga mbele kwa amani.” alisema Flavin.

Stallone na Flavin, kabla ya kutengana kwao hivi karibuni walisherehekea kumbukumbu ya miaka 25 ya ndoa yao, (25th wedding anniversary).

Kwa kipindi chote cha maisha ya ndoa yao, wawili hao wamebarikiwa kupata watoto watatu ambao ni Scarlet, 20, Sistine, 24, na Sophia, 25.

Kenya:Ruto amtunishia misuli Odinga
Vanessa Mdee 'aamsha popo' za Mziiki hadharani