Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Naomi Ireri, raia wa Kenya amesimulia namna ambavyo penzi la usiku mmoja bila kutumia kinga kwenye nyumba ya wageni ya hali ya chini iliyopo kichochoroni lilivyogharimu maisha yake.

Naomi ameeleza kuwa uamuzi wake wa dakika chache ndani ya kuta nne za nyumba hiyo iliyolenga kupokea na kuwapa malazi wageni, ulimgharimu yeye mwenyeji wa eneo hilo baada ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi.

Naomi amesimulia alivyokutana na kidume mmoja mgahawani jijini Nairobi, akamteka kimahaba kwa muonekano wake na jinsi alivyokuwa na uwezo wa kuzungumza akisindikiza neno na tabasamu.

Mrembo huyo ameeleza kuwa anajutia kwakuwa ukweli ni kwamba kwenye umri wa miaka 30, vijana karibu wote huvutia na hata wasio na mvuto wa asilia hutafuta namna ya kufanya wavutie.

Anasema alikutana kwenye steji ya magari na kisha wakajikokota kwenye chumba kimoja cha anasa kilikuwa cha hali ya chini sana, na katika chumba hicho penzi lilishika kasi usiku mzima bila wawili hao kutumia kinga.

“Alinipeleka kwenye ‘Lodge’ ambayo kwanza ilikuwa ya kiwango cha chini sana kwenye mtaa ulio vichochoroni hata siwezi nikakumbuka,” amesema Naomi wakaki akisimulia mkasa huo.

Baada ya kujipa raha usiku huo na kukata kiu yao ya mahaba, wawili hao waliachana siku iliyofuata na hawakuwahi kuonana tena.

Na baada ya muda, alikutana na mwanaume mwingine na kushirika penzi ambapo alibeba ujauzito.

“Baada ya kupimwa nikiwa mjamzito, nilipatikana na virusi. Nikafikiri ni baba ya mtoto wangu alikuwa ameniambukiza lakini kumbe sivyo. Yeye alipimwa na kupatikana hana virusi. Ndipo nikakumbuka usiku ule mmoja na nikajua ni hapo niliambukizwa kwani sikuwa nimeshiriki penzi na mtu mwingine,” amesema.

Alipompigia simu jamaa huyo wa usiku mmoja, alisema waende kupimwa pamoja na hivyo kujua kwa kweli ni yeye alimwachia mzigo wa kuishi maisha yake akimeza dawa za kumaliza makali ya ugonjwa huo.

Alisema sababu yake ya kujitokeza na kuzungumza ni kutoa ushauri kwa wapenzi wazingatie kutumia kinga.

“Wasichana wengi huogopa na kufikiria tu mimba, lakini nataka wajue kuna hatari zaidi. Bebeni mipira ya kinga kwenye mikoba yenu,” ameshauri Naomi.

CCM Yakiri changamoto mchakato kura za maoni
Ujumbe wa Diamond, Lulu kwenye sherehe ya Uwoya…‘tumechoka/zaidi yao’