Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola, amefunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu, ambao ulipelekea kuondolewa kwenye benchi la ufundi, wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Ulaya, usiku wa kuamkia leo.

Guardiola alimbwatukia mwamuzi Antonio Mateu Lahoz aliyechezesha mchezo huo uliomalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja, na kufanikiwa kusonga katika hatua ya nusu fainali.

Guardiola alifikia hatua hiyo wakati wa mapumziko, kufuatia kukasirishwa na maamuzi ya kukataliwa kwa bao la Manchester City, ambalo lilifungwa na mshambuliaji wa pembeni Leroy Sane, dakika chake kabla ya dakika 45 za kwanza kumalizika.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania amefunguliwa mashataka kwa mujibu wa kifungu cha 69(1) cha kanuni za nidhamu za shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), ambacho kinaeleza namna ya kuwasilisha malalamiko kwa mwamuzi endapo kutatokea utata mchezoni.

UEFA pia wamefungua mashataka dhidi ya klabu ya Liverpool, kufuatia mashabiki wao kuwasha mafataki wakati wa mchezo, pamoja na kutupa vitu kwenye sehemu ya kuchezea wakati mchezo ukiendelea.

Mshataka yote mawili yatasilikizwa na kamati ya nidhamu ya UEFA, Mei 31.

Katika mchezo huo Liverpool walifanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao matano kwa moja, ambao unatokana na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri waliouvuna kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliounguruma juma lililopita uwanja wa Anfield.

Video: Rais Dkt. Magufuli azindua Taasisi ya Jakaya Kikwete
Young Africans yashikwa Dar es salaam