Kocha mkuu wa Bayern Munich, Pep Guardiola amewasili nchini Kenya kwa safari binafsi ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya utalii.

Guardiola alitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata (JKIA) akiwa ameongozana na mkewe Cristina Serra, na watoto wao Maria Guardiola, Marius Guardiola na Valentina Guardiola.

Baada ya kuwasili, kocha huyo anayeheshimika sana barani Ulaya alijipiga picha marufu kama ‘selfie’ na mashabiki wake raia wa Kenya ikiwa ni pamoja na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Joho amesema Guardiola amefurahi kufika nchini Kenya na atakuwepo hadi mwaka mpya.

“Amefurahi sana kufika Kenya, atakuwepo hadi baada ya mwaka mpya ila amesema atahitaji utulivu kwa ajili kupumzika na familia yake,”alisema Joho.

Gavana Joho amemwalika kocha huyo anayeondoka Bayern kutembelea fukwe maridhawa za Mombasa.

Ni Leicester City Vs Manchester City
Rufaa Ya Denis Cheryshev Yapigwa Teke