Meneja wa klabu ya Man City Pep Guardiola, ameuweka rehani unahodha wa kikosi chake baada ya kuwataka wachezaji kujadili na kuafikiana juu ya nani atawaongoza kwa msimu ujao wa ligi.

Man City imekua ikiongoza na Vincent Kompany, kwa misimu kadhaa lakini kwa agizo lililotolewa na Guardiola inaonyesha kuna nafasi finyu kwa beki huyo kutoka nchini Ubelgiji kurejeshewa heshima ya unahodha.

Kompany amekua katika wakati mgumu wa kucheza mfululizo michezo ya klabu ya Man City karibu kila msimu, kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo humuandama, hivyo hali hiyo huenda ikamnyima nafasi ya kuchaguliwa kuwa nahodha wa kudumu kikosini.

Guardiola aliwathibitishia waandishi wa habari alipozungumza nao nchini China, ambapo kikosi chake kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi, baada ya kuulizwa kuhusu uhakika wa Kompany kuendelea kuwa nahodha wa kikosi chake.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania alisema, tayari ameshawataka wachezaji wake kukaa na kujadili kwa kina kuhusu suala hilo, na haoni sababu yeye kama mkuu wa benchi la ufundi kuwachagulia nahodha.

“Suala hili lipo kwa wachezaji wenyewe, wanapaswa kuchagua nahodha,” Alisema Guardiola.

“Sitowaingilia katika maamuzi yao kwa sababu jukumu la nani anapaswa kuwaongoza wanapokua uwanjani lipo mikonini mwao. ” aliongeza Guardiola

Hata hivyo imeanza kuhisiwa huenda nahodha mpya wa Man City akatajwa miongoni mwa wachezaji kama Joe Hart, Yaya Toure, Pablo Zabaleta na Sergio Aguero.

Szczesny Kurudishwa Stadio Olimpico
Alexandre Pato Kucheza Soka Hispania