Kocha Mkuu wa  Manchester City, Pep Guardiola ametamba kuwa kwa sasa anataka kuipa timu hiyo matatji matatu ‘treble’ ikiwa ni baada ya kubeba mataji mawili hadi sasa.

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya Man City kubeba ubingwa wa FA juzi Jumamosi (Juni 03) dhidi ya wapinzani wao Manchester United kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Wembley.

Ubingwa huo unakuwa taji la pili ambalo Man City wametwaa kwa msimu huu baada hivi karibuni kubeba ubingwa wa Premier.

Kwa sasa City wanasubiri kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA’ na kama watachukua taji hilo watakuwa wameweka rekodi ya kuchukua mataji matatu ‘treble’ kwa msimu mmoja.

Baada ya mechi Guardiola alisema: “Ni kitu kizuri kwetu kubeba ubingwa huu wa FA mbele ya majirani zetu. Najua tumewapa mashabiki zawadi nzuri ya kushinda mbele ya majirani zetu.

“Sasa tunaweza kuzungumzia kuhusiana na mataji matatu ‘treble’. Tuna mchezo mmoja mbele yetu kabla ya kutimiza hilo. Nimewaambia wachezaji waongeze presha wao binafsi kama watataka kubingwa ubingwa wa Ulaya.”

Usafi uwe sehemu ya maisha yetu - Mavunde
Uganda yaomboleza vifo vya Wanajeshi wake 54