Meneja wa klabu ya Man City, Pep Guardiola ameendelea kusisitiza suala la usajili wa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Schalke 04, Leroy Sane pamoja na beki wa England na klabu ya Everton John Stones.

Guardiola alisisitiza usajili wa wawili hao, alipozungumza na waandishi wa habari nchini China, ambapo kikosi chake jana kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund na kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati sita kwa tano, baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania, alisema ana matarajio makubwa ya kuwasajili wachezaji hao, baada ya kuthibitishiwa na uongozi wa Man City juu ya kutengwa kwa kiasi cha Pauni milion 92, ambacho kinaaminiwa kitatosha kuwahamisha kutoka kwenye klabu zao.

“Sane bado ni mchezaji wa Schalke. Kama atafanikiwa kujiunga nasi, nina uhaikika atakua ni mwenye furaha wakati wote. Na kama ataamua kubaki na klabu yake, nitaheshimu maamuzi yake na pia itakua ni furaha kwa mashabiki wa Schalke,” Guardiola alisema mbele ya waandishi wa habari.

“Haki kadhalika kwa Stones, ni suala hilo hilo, kama ilivyo kwa Sane – bado ni mchezaji wa Everton. Na kila mmoja anefuatilia soka anajua tunavyojitahidi kutaka kumsajili.”

 

Sane, mwenye umri wa miaka 20, amekua katika rada za Man City tangu walipoingia mkataba na Guardiola mwishoni mwa msimu uliopita na ada yake ya usajili inatajwa kufikia Pauni milion 42.

Kwa upande wa Stones, mwenye umri wa miaka 22, anaamiwa atatosha katika nafasi ya ulinzi ya Man City kufuatia mambo mazuri anayoyafanya akiwa na klabu yake ya Everton, na ada yake ya usajili ni Pauni milioni 50.

Jurgen Klopp: Siwezi Kumsajili Mchezaji Kwa Milion 100
Bastian Schweinsteiger Kuondoka Old Trafford