Meneja mpya wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola ameanza mipango ya kufanya usajili kwa ajili ya msimu wa 2016-17, ambao umepangwa kuanza mwezi August mwaka huu.

Guardiola ambaye mwishoni mwa juma lililopita alimalizana na FC Bayern Munich, baada ya mchezo wa kuwania kombe la soka la nchi hiyo dhidi Borussia Dortmund, amepanga kuanza na usajili wa kiungo Ilkay Gundogan.

Kiungo huyo kutoka nchini Ujerumani, amekua kivutio kikubwa cha meneja huyo kutoka nchini Hispania na alikaribia kusaini mkataba na Man city mwezi uliopita, lakini kikwazo kikawa majeraha ya goti yaliyomkabili.

Gundogan, bado ana mkataba na klabu ya Borussia Dortmund hadi mwaka 2017.

Ada yake ya uhamisho inatajwa kuwa Euro milioni 26, na endapo atafanikiwa kujiunga na Man city, atapatiwa kiasi cha Euro milioni 2 kama mgao wake ulioainishwa kwenye mkataba.

Leicester City Wamuweka Sokoni Jamie Vardy
Mourinho Afungasha Kila Kilicho Chake Jijini London