Meneja wa klabu ya Man City Pep Guardiola, amewafariji jirani zao Man Utd kwa kuwaambia wanaweza kumaliza katika nafasi ya nne pamoja na kutokuwa na matokeo mazuri katika ligi kuu nchini Uingereza.

Mspania huyo ambaye klabu yake ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu alisema “Kwa wanavyocheza sasa bado naamini watamaliza nafasi ya nne niliangalia mechi zao dhidi ya Stoke, Burnley na nyingine pale Old Trafford walistahili kushinda mechi hizo lakini soka ndio lipo hivyo”.

Guardiola alisema kuwa United wana wachezaji wazuri na wana historia na makocha wanaoweza kuwapeleka hapo, bado ni safari ndefu kugombania ubingwa na haitokuwa rahisi kutomaliza nafasi ya nne.

Bocco: Tutakaa Nafasi Nzuri Raundi Ya Pili
Mats Hummels Amsihi Jose Mourinho