Meneja wa Man City  Pep Guardiola amesema angependa kumtumia kiungo kutoka nchini Ivory Coast Yaya Toure, katika mchezo wa mzunguuko wa tano wa kombe la ligi ambao utakutanisha na mahasimu wao Man Utd katika uwanja wa Old Trafford.

Guardiola alionyesha dhamira hiyo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo wa hii leo, lakini bado akasisitiza msimamo wake wa kutaka kusikia kiungo huyo anaomba radhi kufuatia sakata lililoibuka mwezi mmoja uliopita dhidi ya wakala Dimitri Seluk.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania alilazimika kumzungumzia Yaya katika mkutano huo, baada ya kuulizwa swali kuhusu uwezekano wa kumtumia, lakini ilidhihiri bado kuna tatizo.

“Ningependa kumtumia Yaya, niamini mimi, ningetaka iwe hivyo, lakini unafahamu tatizo linaloendelea.” Alijibu Guardiola

Wakala wa Yaya Toure (Dimitri Seluk) aliwahi kuzungumza katika vyombo vya habari kuhusu kuchukizwa na mpango wa Guardiola wa kushindwa kumtumia mchezaji wake, na alifikia hatua ya kusema jambo hilo ni sawa na udhalilishaji.

Kauli hiyo ilipokelewa tofauti na Guardiola na ndipo alimtaka Toure na wakala wake waombe radhi hadharani, na kama hawatofanya hivyo mchezaji huyo asahau kucheza katika kikosi cha Man City chini ya utawala wake.

Wanahabari Wa Ufaransa Wamkera Wakala Wa Marko Verratti
EFL Yazidi Kuchanja Mbuga, Tano Zatangulia Robo Fainali