Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Croatia Ivan Perisic, amerejea Inter Milan akitokea kwa mabingwa wa Barani Ulaya FC Bayern Munich alipokua anatumika kwa mkopo.

Meneja wa FC Bayern Munich Hansi Flick amethibitisha kuondoka kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, baada ya kutumika klabuni hapo kwa msimu 2019–2020.

Perisic aliondoka Inter Milan kwa mkopo wa Euro Milioni 5 huku, Munich wakipewa sharti la kumnunua kwa Euro milioni 20, endapo wangevutiwa na kiwango chake.

Hata hivyo mpango wa kiungo huyo kusajiliwa moja kwa moja kwa mabingwa hao wa Ujerumani ulishindikana, baada ya mazungumzo ya pande hizo mbili kugonga mwamba, hasa kwenye kipengele cha kushushwa kwa ada yake ya usajili.

Mbali na Perisic, Hansi Flick amethhibitisha kuondoka kwa wachezaji wengine kama Alvaro Odriozola alierejea kwa mabingwa wa Hispania Real Madrid na Philippe Coutinho alierejea FC Barcelona.

Perisic amecheza michezo 35 na kufunga mabao manane akiwa na Bayern Munich na kuchangia kutetea taji la Bundesliga na kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA).

Kiongozi wa upinzani akamatwa - Belarus
Maalim Seif atakavyopambana na wanaompinga