Peter wa P Square amerusha karata yake ya utabiri kwa ngoma mpya ya Vanessa Mdee ‘Kisela’ aliyopewa shavu kwa mara ya kwanza na msanii wa kike wa Tanzania.

Pacha huyo wa kundi la Nigeria la P Square ambaye kwenye video ya wimbo huo ameonesha uwezo mkubwa wa kuigiza sambamba na Vanessa kwenye penzi lao la kisela, amesema wimbo huo tayari umetusua kwa asilimia 100.

“It’s finally out! KISELA @vanessamdee FT #MrP @peterpsquare I so much love this song and am 100% sure Issa Hit?! Enjoy! #Kisela,” ameandika Peter kwenye Twitter akiambatanisha kipande cha video kinachomuonesha Vanessa akimnasa kibao.

Peter anaeleza kuwa hatimaye wimbo huo umetoka, anaupenda sana na kwamba ana uhakika utatusua.

Kisela ni wimbo mpya wa Vanessa ambao video yake imeongozwa na Clarence wa Capital Dream Pictures.

Akizungumzia wimbo huo jana kwenye XXL ya Clouds FM, Vanessa alisema kuwa maudhui yanaeleza jinsi ambavyo mrembo anaweza kujikuta amezama kimapenzi na mwanaume akijua amefika kumbe mwenzake anafanya ‘kisela’ tu.

Video ya ‘Kisela’ imekamilishwa katika jumba la mazoezi (gym), ikiwaonesha wawili hao wakiwa wanafanya mazoezi kama wapenzi lakini wakati mwingine wanagombana. Mwisho Vanessa anamkuta Peter akiwa na mwanamke mwingine ndani ya eneo hilohilo la mazoezi na anaamua kujiondoa.

Tiba ya kisonono yavumbuliwa
Mpina aitaka NEMC kukichunguza kiwanda cha ANBANGS