Dunia imekuwa kijiji na wakati mwingine ni kama mtaa mmoja mkubwa hivi..! Siku chache baada ya Diamond Platnumz kuanika tuhuma nzito kuwa Zari The Boss Lady alikuwa akichepuka na mwanafamilia wa P-Square, Peter Okoye aka Mr. P, mwimbaji huyo asema jambo kwa mara ya kwanza.

Diamond aliibua tuhuma hizo alipokuwa anafanya mahojiano na radio yake ya Wasafi katika kipindi cha Block 89 wiki hii ambapo alidai kuwa alithibitisha kupitia simu ya mama watoto wake huyo kuwa alikuwa na uhusiano na kimapenzi na Peter.

Watu wa kijiji cha dunia ya mtandaoni walihakikisha wanamfikishia ujumbe kwa haraka Peter kupitia Instagram na Twitter, na aliupata kwa wakati kama mtu aliyekuwa nje Ofisi za Wasafi Media, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Peter ambaye alishafunga pingu za maisha, jana alizungumzia kwa mara ya kwanza tuhuma hizo alipofanya mahojiano na radio moja nchini Nigeria alipokuwa kwenye harakati za kutambulisha wimbo wake mpya wa ‘One More Night’.

Mwimbaji huyo aliziweka kando tuhuma hizo na kudai kuwa ni upumbavu ambao hataki uvuruge harakati zake za kutambulisha wimbo.

“Kwakweli sifahamu wanachozungumzia, siwezi na sitasema kitu chochote, tafadhali nina ngoma mpya na sitaki kuvurugwa. Sitaki kuzungumzia tuhuma za Diamond, kwa hakika ni upumbavu,” Tafsiri ya majibu ya Peter.

Wakati huohuo, kupitia mitandao ya kijamii, ingawa ameshakanusha tuhuma hizo za Diamond, Zari ameendelea kuonesha kuvutiwa na wimbo mpya wa Peter na kuupigia ‘promo’ kubwa hata anapokuwa kwenye mapozi makali kitandani.

Katika post yake moja alimsifia vikali Peter kuanzia muonekano wake, umbo, kuwa na sifa za kuwa mume na hata jinsi anavyojua kucheza.

Ni kama drama ya Zari na Diamond haiwezi kuisha leo kama ile ya Isidingo. Kikitoka kitu vinaingia vitu.

Kwa upande mwingine Zari ameendeleza vita ya michambo na Mange Kimambi, Diamond anaendelea kupaa na views pamoja na shows zinazotokana na mapokezi ya wimbo wake mpya ‘The One’. Hadi sasa wimbo huo umeshaangaliwa mara zaidi ya milioni mbili na laki tisa (2,900,000) ndani ya siku sita.

Rais Magufuli atoa siku saba kwa wakuu wa mikoa inayodharisha dhahabu
Watu 11 wakamatwa, mauaji ya Daktari wa Ebola DRC

Comments

comments