Inawezekana na wewe ni mmoja wa watu wanaojiuliza kwa nini wasanii wa kampuni ya Endless fame ambayo inasimamiwa na Mrembo Wema Sepetu, hawaonekani wakifanya vizuri kama ilivyokuwa ikifikiriwa.

Mirror na Alli Luna walitabiriwa kuwa wasanii watakaofanya vizuri sana kipindi hiki ambacho Mkurugenzi wa Endless fame bado anamvuto mkubwa sana kwa mashabiki wake.

Katika kipindi cha xxl cha Clouds fm jumatatu hii  Wema amefunguka kwa nini wasanii wake hawakufanya vizuri kama ambavyo ilitarajiwa.

“Naweza kusema kuwa kwasababu muda mrefu sana nimemwachia Petit Man akifanya hiyo kazi na sidhani kama alikuwa anaitendea haki kwahiyo ‘let us another six month tusimame sisi kama sisi kwasababu ujue kwenye vitu kama hivi kumtrust mtu labda afanye hiki may be unaweza ukawa unamsapoti afanye any then mwisho wa siku hafanyi unajua kuna vitu vingine vinaingiliana vya kibinaadamu tu,” alisema Wema.

Hata hivyo aliyekuwa Meneja wa wasanii hao kutoka endless fame Petitiman Wakuache ameshaachana na kampuni hiyo na kwa sasa ni Msimamizi wa lebo ya LFLG inayowasimamia wasanii Bilnass pamoja na Nuh Mziwanda.

Video: Mpango wa Usambazaji Umeme Tanzania Nzima Wazinduliwa
Tanzania Yathibitisha Ushiriki Wa Beach Soccer