Mlinda mlango kutoka Jamuhuri Ya Czech na klabu ya Arsenal, Petr Cech amethibitishwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo ya vizuia mkoni vya dhahabu (Golden Glove) katika ligi ya nchini England.

Cech, ambaye alijiunga na Arsenal mwanzoni mwa msimu huu akitokea Chelsea, amepata nafasi hiyo baada ya mlinda mlango wa Man Utd, David de Gea kuruhusu bao katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya AFC Bournemouth waliokubali kichapo cha mabao matatu kwa moja.

Cech alikua akisubiri matokeo ya mchezo huo ili kufahamu kama atapata mpinzani katika tuzo hiyo, kufuatia sifa aliyojizolea ya kutokuruhusu kufungwa bao hata moja katika michezo 16 miongoni mwa michezo yote ya ligi ya England aliyocheza msimu huu.

Mpinzani wa karibu wa Cech alikua De Gea ambaye hakuruhusu kufungwa katika michezo 15, miongoni mwa michezo yote ya ligi aliyochezea msimu huu.

Endapo mlinda mlango huyo kutoka nchini Hispania, kama angefanikiwa kuzuia kufungwa katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo angefikisha idadi ya michezo 16 sawa na Cech na huenda kanuni nyingine za kumsaka mshindi wa tuzo ya vizuia mkono vya dhahabu (Golden Glove) zingetumika.

Orodha ya makipa wa klabu za ligi ya nchini England ambao walikua wakipambana katika tuzo ya vizuia mkono vya dhahabu (Golden Glove) msimu wa 2015-16.

Petr Cech (Arsenal) 16
Joe Hart (Man City) 15
David de Gea (Man Utd) 15
Kasper Schmeichel (Leicester) 15
Hugo Lloris (Tottenham) 13
Heurelho Gomes (Watford) 11
Simon Mignolet (Liverpool) 11
Jack Butland (Stoke) 10
Lukasz Fabianski (Swansea) 9
Adrian (West Ham) 9

Orodha ya makipa wa klabu za ligi kya nchini England ambao wamewahi kutwaa tuzo ya vizuia mkono vya dhahabu (Golden Glove).

2014/15 Joe Hart (Man City) 14
2013/14 Wojciech Szczesny (Arsenal) & Petr Cech (Chelsea) 16
2012/13 Joe Hart (Man City) 18
2011/12 Joe Hart (Man City) 17
2010/11 Joe Hart (Man City) 18
2009/10 Petr Cech (Chelsea) 17
2008/09 Edwin van der Sar (Man Utd) 21
2007/08 Pepe Reina (Liverpool) 18
2006/07 Pepe Reina (Liverpool) 19
2005/06 Pepe Reina (Liverpool) 20
2004/05 Petr Cech (Chelsea) 21

 

Yondani Amrudisha Nadir Haroub Taifa Stars
Louis Van Gaal Awafikishia Ujumbe Zomea Zomea

Comments

comments