Malinda mlango wa klabu ya Arsenal, Petr Cech amekubalia yaishe kufuatia mwenendo wa kikosi cha klabu hiyo kutoridhisha kwenye michezo ya kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Cech amekubali kwamba ni ngumu kwa The Gunners kumaliza msimu wakiwa juu ya wapinzani wao wa karibu Tottenham ambao wamewaacha kwa point nne.

Mlinda mlango huyo ambaye alisajiliwa na Arsenal mwanzoni mwa msimu huu akitokea Chelsea, amesema kutokana na hali halisi kwake habishi jambo hilo na anaamini itakua fundisho kwa kila mmoja klabuni hapo.

Amesema kutokea kwa jambo hilo ni kama pigo kwao lakini kwa upande mwingine huenda likawa jambo jema kwa akuamini utakua mwanzo mzuri wa kuanza kujiandaa na msimu mpya wa ligi ili kujinusuru na yanayotokea sasa.

“Sidhani kama itawezekana kumaliza juu ya Spurs, kama kuna mtu anaamini hivyo utakua ni utashi wake binafsi, lakini sio kwangu maana tumeshajiharibia kabisa”. Alisema Cech mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Sunderland

“Inaonekana ilishazoeleka vibaya kwamba Spurs hawawezi kumaliza juu ya Arsenal na hilo ndilo limetugharimu kutokana na mazoea ambayo hayana msingi wowote” aliongeza Cech

Kikosi cha Arsenal tangu kilipoanza kuwa chini ya meneja Arsene Wenger mwaka 1996, hakijawahi kumaliza chini ya Spurs na kama itatokea msimu huu itakua ni mara ya kwanza katika historia ya The Gunners kwa kipindi cha miaka 19.

Matokeo ya bila kufungana yaliyopatikana jana dhidi ya Sunderland, yanaifanya Arsenal kufikisha point 64, sawa na Man City ambao wapo katika nafasi ya tatu kwa kuwa na uwiyano mkubwa wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Spurs wapo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya nchini England baada ya kujikusanyia point 68, na hii leo wanapambana na West Bromwich Albion huko kaskazini mwa jijini London.

Video Mpya: Colors of Africa - Mafikizolo Feat. Diamond & Maphorisa
Donald Trump: Nikishindwa Hamtaniona Tena