Beki wa Man Utd Phil Jones, amemkaribisha Victor Lindelof aliyesajiliwa klabuni hapo usiku wa kuamkia leo akitokea  SL Benfica ya Ureno.

Jones, amesema ujio wa beki huyo kutoka nchini Sweden, utaongeza chachu ya ushindani katika safu ya ulinzi wa Man Utd, jambo ambalo anaamini litakua zuri kwa mafanikio ya klabu hiyo ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya sita, kwenye msimamo wa ligi ya England.

Lindelof mwenye umri wa miaka 22, alikua na mafanikio makubwa nchini Ureno msimu uliopita, huku akikosa michezo sita kati ya 46 aliyocheza kwenye michuano yote waliyoshiriki.

Jones ameongeza kuwa, anaamini katika ushindani, na kila siku suala hilo limekua likimuwezesha kujiamini na kucheza kwa kujituma kwa maslahi ya klabu ama upande wa timu ya taifa.

Msimu uliopita beki huyo kutoka England mwenye umri wa miaka 25, alishindwa kucheza michezo kadhaa, kutokana na majeraha ya mara kwa mara. Alicheza michezo 21 kati ya 64 ya michuano yote waliyoshiriki.

Lindelof anakua mcheza wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Dodoma kinara mimba za utotoni
Mzee Akilimali: Clement Sanga Akijiuzulu, Nitafanya Usajili

Comments

comments