Gwiji wa klabu ya Liverpool, Phil Thompson ameonyesha wasiwasi wa klabu hiyo kupoteza mchezo wake wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali wa Europa League, dhidi ya Borussia Dortmund endapo meneja Jurgen Klopp atabeba dhima ya kumjumuisha kikosini beki kutoka nchini Ufaransa, Mamadou Sakho.

Kikosi cha Liverpool kesho kitakabiliwa na mchezo huo kwenye uwanja wa Westfalen huko nchini Ujerumani, ikiwa ni mtihani mzito kwa Klopp ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Borussia Dortmund kabla ya kutangaza kujiweka pembeni mwaka 2015.

Thompson ameonyesha wasiwasi wa kupoteza mchezo huo, kufuatia udhaifu mkubwa ambao umeonyeshwa na Mamadou Sakho katika siku za hivi karibuni ambapo Liverpool imeshindwa kufungwa bao sambamba na kusaka ushindi katika michezo mitatu aliyopewa nafasi ya kucheza.

Thompson, amesema beki huyo ameshindwa kufanya juhudi za kuzuia kwa asilimia 40 katika michezo hiyo mitatu, hali ambayo imesababisha hali kuwa mbaya kwenye kikosi cha Liverpool ambacho msimu huu kimedhamiria kumaliza kikiwa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Phil ThompsonPhil Thompson

Amesema kasi na ushujaa wa wachezaji wa Borussia Dortmund, unamuogopesha sana juu ya uwezo wa beki huyo mwenye umri wa miaka 26, hivyo ameshauri ni bora njia mbadala zitafutwe kabla kikosi cha The Reds hakijaingia uwanjani.

“Sina uhakika sana kama Sakho ataweza kufanya kinachotarajiwa na mashabiki wengi wa Liverpool, binfasi nimemchunguza na kuona ana mapungufu makubwa katika michezo mitatu iliyopita, hivyo kuna wasiwasi wa kuendelea kupotea zaidi kama atapewa nafasi na meneja Klopp.” Amesema Thompson

“Sakho hupata wakati mgumu anapokuwa katika hali ya kutokujiamini, na hali hiyo humpelekea kuigharimu timu kwa kiasi kubwa, hivyo sishauri atumike katika mchezo wa kesho.” Aliongeza gwiji huyo.

Hata hivyo Thompson ameshauri, Martin Skrtel, apewe jukumu la kuongoza safu ya ulinzi katika mchezo huo, kutokana na kuonyesha umakini tofauti na ilivyo kwa Sakho.

Gardner Habash aleza faida/hasara baada ya kuachana na Lady Jay Dee
Diamond kupiga collabo na Kanye West? Menejimenti zao zawekana sawa