Majogoo wa jiji Liverpool, watalazimika kupambana katika michezo ya mwishoni mwa mwaka huu bila ya kuwa na kiungo mshambuliaji Philippe Coutinho.

Coutinho alifanyiwa vipimo hapo jana na imebainika aliumia kifundo cha mguu, hali ambayo inamlazimu kukaa nje ya uwanja hadi mwanzoni mwa mwaka 2017.

Kiungo huyo kutoka nchini Brazil, aliumia kifundo cha mguu wakati wa mchezo wa ligi ya England dhidi ya Sunderland ambao ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Ripoti ya daktari wa Liverpool imeshauri kuwa, Coutinho apumzike kwa muda wa majuma sita, ambapo atakua akiendelea na matibabu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, atakosa mchezo wa kombe la ligi (EFL Cup) dhidi ya Leeds Utd ambao utaunguruma katika uwanja wa Anfield hii leo.

Michezo mingine ambayo Coutinho hatoshiriki ni dhidi ya West Ham, Middlesbrough, Everton, Stoke, Manchester City pamoja na Sunderland huku kukiwa na mashaka ya kuwakosa Manchester United ambao watawasubiri Liverpool katika uwanja wa Old Trafford Januari 15.

Video: Profesa Ndalichako apingwa kila kona, Chadema sasa ni 'Kata Funua'...
Jose Mourinho Kusimamishwa Kizimbani