Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete amefungua mkutano wa kamati kuu ya CCM kwenye ukumbi wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Ambapo Dkt Kikwete ameeleza kuwa ajenda ya mkutano huo ni yeye kun g’atuka na kumpa nafasi Rais wa awamu tano, Rais John Pombe Magufuli
Katibu mkuu wa CCM, Abdallahaman Kinana akimpokea mwenyekiti mtarajiwa wa CCM, Rais John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiimba wimbo wa CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli akiteta na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.

