Kiongozi wa G-Unit, 50 Cent ameendelea kumuandama Ja Rule ambapo wiki hii amezua jambo kwa kununua tiketi 200 za viti vya mbele vya tamasha la hasimu wake huyo ili viwe wazi.

Ja Rule anajiandaa kufanya tamasha lake kwenye ukumbi mmoja ulioko Texas nchini humo, Novemba 9 mwaka huu.

Ingawa tamasha hilo bado halijafanyika, 50 Cent ameweka picha iliyotengenezwa ikionesha viti vingi vya mbele vikiwa wazi, huku akiwa amekaa peke yake akiangalia tamasha na kwa mbali wanaanza kuonekana watu wengine.

“Nimenunua tiketi 200 za viti vya mbele ili viwe wazi,” aliandika kwenye picha hiyo.

Katika picha nyingine aliyoweka, ameonekana kama vile ni mtu ambaye yuko kwenye tamasha hilo tayari akimpa moyo Ja Rule kuwa aendelee kuimba kwani anafunika.

 

View this post on Instagram

 

LOL?Damn Boy you put on a hell of a show. ?get the strap #bellator #lecheminduroi

A post shared by 50 Cent (@50cent) on


‘Bifu’ kati ya wasanii hao iliyodumu kwa miaka kadhaa na kufifia baada ya Ja Rule kuwa nje ya reli ya muziki wa mafanikio kwa kipindi kirefu, iliibuka tena mapema mwaka huu kupitia Twitter.

Hata hivyo, miezi miwili iliyopita, Eminem alikuwa chanzo cha kurejea kwa mashambulizi zaidi kati ya wasanii hao baada ya kumchana Ja Rule kwenye wimbo wake ‘Kill Shot’ alioutoa kujibu mashambulizi ya rapa Machine Gun Kelly.

Ja Rule alijibu kupitia Twitter akiitaja moja kati ya ngoma zake alizotoa kumchana 50 Cent enzi hizo kuwa ni miongoni mwa ngoma kali za kushambuliana (diss track).

Hatua hiyo ilimuibua tena 50 Cent ambaye ameendelea kumvuruga hadi wiki hii. Mashabiki wengi wa muziki wamemshauri Ja Rule kuachana na 50 Cent kwani hana dogo dhidi ya hasimu wake na anampotezea dira ya mafanikio.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 28, 2018
Serikali kushusha tena rungu kwa Wema, ‘hana utoto, hajitambui’