Kikosi cha klabu ya Al Hilal ya Sudan kimewasili nchini kikitoa mjini Khatoum tayari kwa michuano ya Simba Super Cup, itakayoanza rasmi kesho Jumatano (Januari 27), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Al Hilal wamewasili leo mchana na kupokelewa na wenyeji wao Simba SC, ambao wameandaa michuano ya Simba Super Cup, yenye lengo la kupasha misuli moto kabla ya kuanza kwa nginja nginja za hatua ya makundi Ligi ya mabingwa Barani Ulaya.

Al Hilal watacheza mchezo wa michuano hiyo kesho Jumatano dhidi ya wenyeji wao Simba SC, huku timu nyingine mwalikwa kwenye michuano hiyo TP Mazembe ikitarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam.

Kocha Kaze achukua maamuzi magumu Young Africans
Peter Muduhwa atambulishwa Simba SC