Msanii wa Muziki wa Bongo fleva nchini na mkali wa nyimbo ya ”Seduce me”, Ali Kiba leo hii anafunga ndoa na binti wa Mombasa, Bi Amina Sharif Ahmed na shughuli nzima kuoneshwa katika chaneli ya Azam Tv na Sinema zetu tu.

Alikiba amefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum huko Mombasa na sherehe yake inatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa jubilee uliopo hukuhuko jijini Mombassa na kutarajiwa kuhudhuriwa na watu wasiopungua 450.

Harusi hiyo inafanyika ikiwa na baraka za Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ambapo Alikiba alipata nafasi ya kumtembelea nyumbani kwake na kumueleza juu ya swala lake la kuona.

Alikiba ametumia ukurasa wake wa Instagram kurusha baadhi ya picha ikimuonesha akiwa katika vazi lake la kanzu pamoja na familia yake yaani mama yake na mdogo wake, Abdu Kiba, picha hiyoa ameisindikiza kwa maneno.

”Siku ya leo ndio Mama yangu na baba yangu walifunga ndoa” Alikiba.

Tazama baadhi ya picha zikionesha shughuli hiyo inavyoendelea kufanyika huko Mombasa.

 

Wabunge wapinga uendeshwaji kampeni ya Makonda
Canelo Alvarez afungiwa miezi sita