Shirikisho La Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) pamoja na wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara (Kampuni ya Vodacom) wametimiza ahadi ya kupelekea taji la ubingwa (VPL 2019/20) mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

TFF na TPLB kwa kushirikiana na wadhamini waliahidi kufanya hivyo ili kukamilisha mpango wa kuwakabidhi mabingwa Simba SC taji la ubingwa msimu huu, mara baada ya mchezo dhidi ya Namungo FC ambao utachezwa Uwanja wa Majaliwa leo jioni.

Tayari taji la ubingwa (Kombe La Ubingwa) limeshawasili uwanjani hapo na kuweka mahala pake, na unasubiriwa muda muafaka kwa Simba SC kukabidhiwa mwali wao.

Kocha Yanga Princess aipania Simba Queens
Joshua Nassari ajiunga na CCM, azungumzia mpango wa ubunge