Kikosi cha Azam FC kimeonesha heshima kwa Mabingwa wa Tanzania Bara mara nne mfululizo Simba SC, kwa kuwapigia makofi ya pongezi.

Azam FC imefanya hivyo ikiwa ni kukamilisha sehemu ya kanuni za Ligi Kuu ambazo huitaka timu bingwa kuoneshwa heshima hiyo, pindi inapojitangazia ubingwa, huku ikisaliwa na michezo kadhaa.

Tukio la heshima kwa Simba SC limefanyika kabla ya kuanza kwa mchezo wa Mzunguuko wa 33 wa Ligi Kuu unaoendelea Azam Complex Chamazi.

Namungo FC ambayo itacheza dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Mzunguuko wa 34 ambao utakua wa mwisho kwa msimu huu 2020-21, nayo italazimika kuonesha heshima kwa wachezaji wa Simba SC siku ya Jumapili (Julai 18).

Dogo Janja akataa kutumia 'ROBOTI'
Biashara Utd kucheza Kombe la Shirikisho Afrika