Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho Septemba 27, 2018 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Daraja la Juu ‘flyover’ katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere katika eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amesema Flyover hiyo itapunguza changamoto ya msongamano barabarani iliyokuwa inaleta hasara ya Tsh. Bilioni 400 kwa mwezi.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewaalika viongozi wa upinzani kwenda kushuhudia tukio hilo na kuwa atawaweka sehemu maalumu ya kukaa akiamini wao ndio wanaongoza kuponda maendeleo hayo.

Mnamo Septema 15, 2018 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Abbas Hassan, alithibitisha kuwa Serikali imeruhusu barabara zianze kutumika kwa  majaribio hadi pale uzinduzi utakapofanyika.

Barabara hiyo ya juu ni ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake umegharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 93.44 zimetolewa na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania imetoa shilingi Bilioni 8.3.

Barabara hiyo ya juu ina njia nne na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

 

 

Pape Cheikh Gueye asubiri wito wa Luis Enrique
Video: Ben Pol aachia ngoma mpya 'Ntala nawe' Monalisa yumo