Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wameendelea na kikao chao kwa siku ya pili jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 – 13 Machi, 2021 kwa njia ya mtandao.   

Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho unaongozwa na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban.   

Katika Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri wa SADC, ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi.

Mwenyekiti wa Sasa katika Jumuiya ya SADC ni Msumbiji na ndiye atakayeongoza majadiliano ya Mkutano huu.

Rage: Simba SC wana haki ya kupewa alama tatu, magoli mawili
Mlipuko waua zaidi ya 90 Guinea