Katika hali ya kushangaza, Sherehe moja ya harusi nchini India iliyofanyika Machi 8 mwaka huu (Siku ya Wanawake Duniani), iligeuka kuwa uwanja wa mapambano baada ya bibi harusi kumshushia bwana harusi kipigo cha nguvu mbele ya waalikwa baada ya kuonekana kwenye tukio hilo akiwa amelewa.

Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Ranjeet Kumar Kamat alimshambulia mumewe huyo mtarajiwa kwa kumpiga usoni na kisha kumrushia viatu kabla ya kumfungia vingine shingoni.

Kwa mujibu wa Dailymail, baada ya kichapo hicho, familia ya bibi harusi wakishirikiana na mwanamke huyo walimfungia kijana huyo chumbani hadi pale familia ya kijana huyo ilipokubali kurudisha mahari, kwani kwa tamaduni za ukoo huo, wanawake huwalipia mahari wanaume.

Bwana harusi, aliyevalishwa viatu shingoni

Bwana harusi, aliyevalishwa viatu shingoni

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Khutauna – Natoli kilichopo katika wilaya ya Madhubani, wameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii (Siku ya Wanawake Duniani), ambapo bwana harusi huyo alienda kwenye baa ya jirani akiwa na binamu yake na baadae walirejea wakiwa wamelewa.

Baada ya kurejea, bwana harusi huyo aliendelea kuomba bia mbele ya wageni waalikwa ba baada ya kukatazwa alianza kulazimishwa. Kitendo hicho kilimchukiza bibi harusi ambaye aliamua kumkataa palepale na kuahirisha harusi.

 

 

 

Rafael Benitez Kuwa Mbadala Wa Steve McClaren
Herve Renard Ataja Kikosi Cha Morocco